School Report

Your ads will be inserted here by

Easy Plugin for AdSense.

Please go to the plugin admin page to
Paste your ad code OR
Suppress this ad slot.

TAARIFA YA SHULE KWENYE MKUTANO WA WAZAZI ULIOFANYIKA TAREHE 10/08/2014

 

 

 

  1. UTANGULIZI

Ninapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wazazi na walezi kwa ushirikiano wenu ambao umetuwezesha kutekeleza majukumu yetu kwa kipindi chote cha muhula wa kwanza.

Nimatumaini yetu kuwa mtaendelea na moyo huo huo kwa kipindi cha muhula wa pili.

Taarifa hii inalenga kutoa tathmini ya maendeleo ya Taaluma, Mahafali ya wanafunzi wa shule ya Awali na ya wanafunziwa wa darasa la 7 mwaka 2014.  Bajeti ya mahafali, Programu ya masomo ya kujirekebisha na masomo ya usiku (Night Preps).

 

  1. MAENDELEO YA TAALUMA

Katika kuhakikisha kuwa shule inaendelea kupata ufaulu endelevu kitaaluma programu ya masomo ya usiku (Night preps) kwa wanafunzi wa bweni imeanzishwa.  Programu hii inalenga kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji ya usaidizi wa karibu kitaaluma.  Hivyo walimu wa masomo huwasaidia wanafunzi kulingana na masomo wanayofundisha kila siku.

  1. Mitihani ya ndani

Wanafunzi wetu mbali ya kufanya majaribio na mazoezi mbalimbali ya masomo wanayofundishwa.

Pia wameshafanya mitihani mine (4) mikubwa yaani miwili ya mwezi na mingine miwili (2) ya muhula (Nusu muhula na mwisho wa muhula)

Kwa kipindi cha miezi (6) yaani Januari hadi Julai hali ya ufaulu wa shule ulikuwa kama ifuatayo:-

 

Shule ya awali mpaka darasa la 2 Matarajio90% na zaidi Ufaulu halisi85.7%
Darasa la 3 – 7 75% na zaidi 66.1%
Wastani wa shule 75.9%

 

Wastani wa shule ni 75.9% sawa na daraja la B. Matarajio yetu ifikapo mwisho wa mwaka wa masomo wastani wa shule uwe daraja la A yaani usipungue 81%.

  1. Mitihani ya nje

Wanafunzi wa darasa la nne (4) mpaka sasa wameshafanya mitihani miwili (2) ya Utamilifu (Mocks) ya Mkoa.  Mitihani hii walifanya Mei na Julai 2014.  Kiwango cha ufaulu kilikuwa 68.2% sawa na daraja  B.

Kwa upande wa darasa la saba hadi sasa wamefanya mitihani ya nje mitano (5) yaani ya Utamilifu (Mocks) ambayo ni wa Kata, Wilaya, Mkoa na mingine miwili (2) ya Mkoa ya shule zisizo za serikali (NGOPSO).

 

Hali ya ufaulu kwa mitihani ilikuwa kama ifuatavyo:-

Mitihani Wastani ( %) Daraja
Kata 59.0 C
Mkoa (Serikali) 73.2 B
Mkoa (NGOPSO) 67.0 B

 

Aidha wanafunzi wa darasa la Saba wamefanya mitihani mingine mitatu(3) ya nje ya kiushindani na shule zingine nakuweza kupata ngao na vyeti.

Pia wanafunzi wetu hawa wamefanya mitihani ya ujarani mwema na shule zifautazo Canosa, Liberman, Daystar, Hope&Joy nakupata ufaulu mzuri. Katika wanafunzi  kumi bora Moga ina wanafunzi watano(5) yaani nafasi ya 1,2, 6 na wawili walioshika nafasi ya 7.

Your ads will be inserted here by

Easy Plugin for AdSense.

Please go to the plugin admin page to
Paste your ad code OR
Suppress this ad slot.

Mitihani hii inalenga kuwajengea wanafunzi wetu uwezo wa kujiamini kabla ya kufanya mitihani ya Taifa na ya usaili wa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.

 

  1. PROGRAMU YA KUJIREKEBISHA DARASA LA SABA 2014

Programu ya darasa la saba inaendelea vizuri.  Wanafunzi wetu wemeweza kusaidiwa na walimu wetu katika masomo yao.  Mpaka sasa wanafunzi wetu wemekiwashafanya mitihani 20 kati ya 20.  (Evaluations) Kiwango cha ufaulu kwa sasa ni wastani 34.9 sawa   69.8% ambayo ni daraja la B.

 

  1. MAHAFALI YA DARASA LA SABA NA YA WANAFUNZI WA SHULE YA AWALI 2014

Mahafali ya darasa la saba (7) na ya wanafunzi wa shule ya awali hatua ya mwisho(PU2) yanatarajiwa kufanyika tarehe 14 Septemba 2014 siku ya Jumapili baada ya mtihani wa Taifa wa kumaliza Elimu ya Msingi.  Mitihani hii itafanyika tarehe 10 na 11 Septemba 2014.

Maandalizi yanaendelea vizuri hususan kitaaluma, Maonyesho, Burudani, kiroho na kisaikolojia.

 

  1. BAJETI YA MAHAFALI 2014

Mahafali ya mwaka huu yatagharimu TZS. 24,000,000/= tofauti na mwaka jana ambapo yaligharimu TZS. 19,023,000/=. Ongezeko hili limetokana na kuongezeka kwa idadi ya watu.

Gharama hizi zitajumuisha chakula, vinywaji (baridi),  Mshereheshaji (MC), picha za kumbukumbu, motisha kwa wafanyakazi, zawadi kwa wanafunzi n.k.

 

 

 

  1. SERA YA KUPANDISHA WANAFUNZI

Sera ya upandishaji wanafunzi toka darasa moja kwenda lingine mwanafunzi hana budi kupata wastani usiopungua 65%.  Taarifa hii imo pia kwenye kitabu cha maendeleo cha mwanafunzi ukurasa wa 7.

Hivyo basi, tunawaomba wazazi na walezi waelewe sera hii na kutoa ushirikiano kwa kuwahimiza watoto kuongeza juhudi masomoni.  Pili, ili kuhakikisha kuwa ufaulu endelevu unakuwepo shuleni na kuendana na ushindani na shule zingine kitaaluma.

Wazazi na walezi wote hawana budi kukubaliana na sera hii.  Kwa kufanya hivi tutaweza kuinua kiwango cha ufaulu toka kiwango cha darasa moja hadi jingine na hatimaye shule nzima.  Hata kauli mbiu yetu inasema “Ubora hupatikana kwa kuchagua”  Aidha juhudi ndio njia pekee itakayotuwezesha kupata mafanikio na ufaulu endelevu kwenye shule yetu.

***Mungu ibariki Moga***

***Mungu ibariki Tanzania***

 

Pamoja tutaijenga Moga.

Taarifa hii imeandaliwa na kusomwa kwenu na

 

Mark  N.  Massangya

Mwalimu Mkuu